Vigezo vya Bima

1. Kigezo cha umri

Mwenye bima ama atayefaidika na bima hii atakuwa na umri usiozidi miaka 75 wakati atakapokutwa na ajali

2. Gharama za bima

Malipo yote yatakayofanyika kutokana na ajali/ maafa yote hayatazidi kiasi cha TSH 35, 000, 000

1. Malipo ya gharama za bima

Malipo yatalipwa moja kwa moja kwa aliyejeruhiwa au mwakilishi aliyechaguliwa kisheria

2. Idadi na maeneo ambapo bima itatolewa kwa mnufaika wa bima

Malipo yote kwa muhusika yatatokana na faida zilizotajwa hapo juu kwa tukio moja tu litakapotokea

3. Gharama za bima katika kampuni

Malipo kamili ya kampuni hayatazidi kiasi kiasi cha TSH 20, 000, 000 kwa mtu mmoja ama kwa aliyekata bima, ama yule atakaefaidika na mpango huu. Kiasi cha TSH 15, 000.000 kitatolewa kwa mtoto aliyesajiliwa na kampuni katika kipindi cha bima

4.Idadi ya magari yatakayonufaika na bima hii

Ikiwa mwenye bima/ ama yule atakayefaidika na bima atakuwa na magari zaidi ya moja katika kampuni atanufaika kutokana bima ya gari moja tu